Leo dawa bure
Mdada kaingia duka la dawa kamkuta mfamasia mwanaume wa makamo hivi;
MDADA: Naomba sumu ya kuulia mtu, nataka kumuua mume wangu si muaminifu
MFAMASIA: Mama mbona unataka kuniweka majaribuni , hiyo sitakuuzia, labda uje na cheti cha daktari hahahahaha……. Mdada akatoa picha inamuonyesha mumewe yuko kitandani na mke wa huyo mfamasia…..
MDADA: Cheti cha daktari hiki hapa
MFAMASIA: Kumbe una cheti, haya unataka kiasi gani cha dawa, na leo tunafanya promo dawa bure