.
mtoto mwenye umri wa miaka 4 Nyambuli Mganga akiwa na kikundi cha sanaa na utamaduni kijulikanacho kwa jina la Utandawazi Theatre Group Matwigha Chalo kutoka Nansole Ukerewe akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ukerewe inayojulikana kwa jina la Obusimbula katika meza kuu ,ambaye amekuwa kivutio kutokana na kucheza kwake mwenyewe bila kuelelezwa wakati maonesho ya 31 ya Tamasha na Sanaa na Utamaduni liliyofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TAsuBA) iliyopo Bagamoyo, mkoa wa Pwani ,. Nyambuli ambaye anarithi utamaduni huo kutoka kwa mama yake, Wiliherimina Kebela . Maonesho hayo yamaeambatana na Sherehe za mahafali ya 23 ya taasisi hiyo zilizofanyika jana(juzi).
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TaSuBa), Profesa Elias Jengo ambaye ni Mhadhili wa taaluma hiyo katika Chuo Kikuu cha Dares Salaam(UDSM),akimpatia cheti mhitimu wa Stashada ya Sanaa na Utamaduni , Charles Kiswaga katika mahafali ya 23 ya yaliyofanyika kwenye ukumbi wa maonesho chuoni hapo. Katikati Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Juma Bakari na kulia ni Mkuu wa Idara ya Taaluma Michael Kadinde