ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BIASHARA
  • Lifestyle
  • BURUDANI
  • MICHEZO
Sunday, April 2, 2023
  • Login
BONGOSWAGGZ
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
    • All
    • Business
    • Politics
    • Science
    • World
    SAKA AIBUKA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI EPL

    SAKA AIBUKA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI EPL

    HOMA YA DENGUE YAIBUKA KWA KASI SUDAN

    HOMA YA DENGUE YAIBUKA KWA KASI SUDAN

    TRUMP AJIBU MASHTAKA

    TRUMP AJIBU MASHTAKA

    MAANDAMANO KENYA YAHISIWA KUWA MAKUSUDI

    MAANDAMANO KENYA YAHISIWA KUWA MAKUSUDI

    KCMC YAPOKEA VIFAA TIBA VYA UPASUAJI

    KCMC YAPOKEA VIFAA TIBA VYA UPASUAJI

    OSCAR PISTORIUS: UWEZEKANO KUACHILIWA MAPEMA KUZINGATIWA

    OSCAR PISTORIUS: UWEZEKANO KUACHILIWA MAPEMA KUZINGATIWA

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • BIASHARA

    The Legend of Zelda: Breath of the Wild gameplay on the Nintendo Switch

    Shadow Tactics: Blades of the Shogun Review

    macOS Sierra review: Mac users get a modest update this year

    Hands on: Samsung Galaxy A5 2017 review

    The Last Guardian Playstation 4 Game review

    Intel Core i7-7700K ‘Kaby Lake’ review

  • Lifestyle
    • All
    • Food
    • Health
    • Travel

    Shooting More than 40 Years of New York’s Halloween Parade

    Why Millennials Need to Save Twice as Much as Boomers Did

    Doctors take inspiration from online dating to build organ transplant AI

    How couples can solve lighting disagreements for good

    Ducati launch: Lorenzo and Dovizioso’s Desmosedici

    23 Celebrity Tweets You Missed From The Golden Globes

    Trending Tags

    • Golden Globes
    • Game of Thrones
    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • BURUDANI
    • All
    • Apps
    • Gadget
    • Mobile
    • Startup

    These Are the 5 Big Tech Stories to Watch in 2017

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • MICHEZO
    • All
    • Gaming
    • Movie

    macOS Sierra review: Mac users get a modest update this year

    Hands on: Samsung Galaxy A5 2017 review

    Heroes of the Storm Global Championship 2017 starts tomorrow, here’s what you need to know

    Harnessing the power of VR with Power Rangers and Snapdragon 835

    Dota 2 and CS:GO top Steam’s 2016 list for most played games

    President Obama Holds his Final Press Conference

No Result
View All Result

Bongoswaggz
No Result
View All Result

JANUARY MAKAMBA: NATAFAKARI URAIS 2015

admin by admin
November 4, 2013
in Uncategorized
Reading Time: 4 mins read
A A
0
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

january_8ae0d.jpg
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema kuwa anatafakari iwapo awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutokana na kuwapo kwa watu wengi hasa ndani ya CCM, wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.
Makamba ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM alisema: “Kwanza ni kweli kwamba kuna ushawishi kuhusu suala hilo kutoka kwa vijana walioko nje na ndani ya chama, wanataaluma, baadhi ya wazee na watu wengine iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja wamekuwa wakinishawishi kugombea kwa muda sasa.”
Aliongeza: “Mwanzoni sikuona uzito sana, yaani sikuzingatia sana, lakini kwa kadiri siku zinavyokwenda ni kwamba ushawishi umekuwa mkubwa na hivyo niseme ni jambo ambalo sasa ninalitafakari kwa kina”.
Alisema ikiwa ataamua kuwania urais, atafanya hivyo wakati mwafaka kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na chama hicho, lakini akasema kwa sasa si wakati wake. Makamba alikuwa akijibu hoja za gazeti hili lililotaka ufafanuzi wake kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba ameanza harakati za kuusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Gazeti hili lilidokezwa kuwa hatua yake hiyo imemwingiza katika mvutano usio rasmi na wanasiasa ambao tayari wameonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini, wakiwamo wale wa kambi ya urais aliyokuwa akidaiwa kuwa mmoja wao.
Awali iliaminika kuwa Makamba alikuwa katika kambi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini wachambuzi wa masuala ya kisisa wanasema ‘katika siku za karibuni mwenendo wake unaashiria kwamba si mmoja wa wanaomuunga mkono kiongozi huyo, bali ni mtu mwenye mipango yake binafsi ya kisiasa”.
Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema mwenendo wa Makamba umewakasirisha baadhi ya wanasiasa hususan wanaomuunga mkono Lowassa ambao mara kadhaa wamesikika hadharani wakimlalamikia kwamba ni msaliti.
Hata hivyo, Makamba katika maelezo yake anasema hajawahi kuwa katika kundi lolote la kumuunga mkono mtu yeyote kwani yeye haamini katika makundi. “Ninaamini katika kundi moja, nalo ni CCM,” alisema.
Aliongeza: “Kwa hiyo mtu yoyote akinikasirikia kwa sababu zozote zile za kisiasa nitamshangaa maana sijawahi mahali popote na kwa namna yoyote kujitanabaisha kwamba mimi nipo kwenye kundi fulani, au kundi la mtu yeyote.”
Sababu za mashaka
Miongoni mwa nyedo zinazotiliwa shaka za mwanasiasa huyo ni hatua yake ya kushiriki katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) uliofanyika Zanzibar ambako pamoja na mambo mengine aligawa simu zaidi ya 100 aina ya Samsung Galaxy kwa wajumbe wa mkutano huo.
Imethibitika kwamba mpango huo ulikuwa ni wake binafsi na haukuwashirikisha waliokuwa wakiamini kwamba wako naye katika harakati za kumuunga mkono Lowassa.
Tukio jingine ni lile la vijana waliojitambulisha kuwa viongozi wa vyuo vikuu nchini kutangaza katika mkutano wao mjini Morogoro kwamba watamwomba Makamba awanie urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, kutokana na kile walichodai kwamba ni matokeo ya kura walizopiga baina ya kiongozi huyo na viongozi wengine vijana; John Mnyika na Zitto Kabwe wa Chadema.
Wapinzani wake wanaamini kwamba tamko la vijana hao zilikuwa mbinu binafsi za Makamba kutaka kuonyesha kwamba naye anakubalika na pengine maandalizi ya kujiengua rasmi kutoka katika kambi yake ya awali.
Wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 14 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Makamba alikuwa Butiama mkoani Mara ambako mbali na kushiriki Ibada ya kumwombea Baba wa Taifa, pia alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kumuenzi kiongozi huyo.
Kuhusu baadhi ya makada wenzake kukasirishwa na mwenendo wake kisiasa, Makamba alisema: “Hata mimi nimesikia kama wewe unavyosema umesikia, inawezekana wanakasirishwa na mvumo maana ndani ya chama chetu watu wanazungumza sana, tena hadharani kwa hiyo katika mazingira hayo taarifa zinaweza kumfikia yeyote kama zilivyokufikia wewe”.
Alitetea hatua yake ya kugawa simu kwenye mkutano wa UVCCM akisema alikuwa akitimiza ahadi aliyoitoa wakati wa semina ya vijana hao Februari mwaka huu mjini Dodoma, pale walipomuomba kuwasaidia ili waweze kutekeleza matakwa ya ushauri wake wa kukitetea CCM katika mitandao ya kijamii.
“Mimi kwa nafasi yangu nikiwa Naibu Waziri wa masuala ya teknolojia, nikiombwa kusaidia lolote katika eneo langu ndani ya chama sioni tatizo ilimradi niwe na uwezo nalo, kwa hiyo nilitimiza ahadi yangu tena kwa uwazi sikufanya kwa kificho,”alisisitiza.
Makamba ni mwanasiasa wa tatu kijana kutajwa kuwa huenda akawania urais, wengine wakiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Wengine ambao wameishaonyesha nia ya kuutaka urais ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Lowassa.
Vita ya urais imekuwa ikikiumiza CCM, ambapo Makamu Mwenyekiti wake (Tanzania Bara), Philip Mangula aliwahi kukaririwa akiwaonya makada wa chama hicho ambao wameanza kupiga mbio za kuusaka uongozi huo kuwa hawatavumiliwa, kwani harakati hizo zimekuwa kichocheo cha mgawanyiko ndani ya chama.
Previous Post

HUZUNI::PICHA ZA KIJANA ALIYEJINYONGA KUKWEPA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE ILIYOANZA LEO,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA.

Next Post

[infographic] Smartphone supremacy: Apple vs Samsung – is it Quality or QUANTITY

admin

admin

RelatedPosts

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, wateja kuzoa Mil. 180/-
Uncategorized

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, wateja kuzoa Mil. 180/-

by iamkrantz
March 31, 2023
0

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paul Chacha pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya...

Read more

Mtanzania aibuka kinara tuzo za uvumbuzi kwenye teknolojia barani Africa

March 31, 2023
ROYAL TOUR YATIKI, NDEGE 3 ZATUA KIA

ROYAL TOUR YATIKI, NDEGE 3 ZATUA KIA

March 31, 2023
BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO WA WAHARIRI MOROGORO

BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO WA WAHARIRI MOROGORO

March 30, 2023
Benki ya NMB Yakabidhi  vifaa vya ujenzi kwa shule ya msingi Sinyaulime na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa (FDC)

Benki ya NMB Yakabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya msingi Sinyaulime na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa (FDC)

March 30, 2023
Naibu Waziri   aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya  michezo

Naibu Waziri   aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya  michezo

March 27, 2023
Load More
Next Post

[infographic] Smartphone supremacy: Apple vs Samsung - is it Quality or QUANTITY

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

Stay Connected test

  • Trending
  • Comments
  • Latest
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Machi 27,2023

March 27, 2023
MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI

MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI

March 28, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023

Habari Kuu Kwenye Magazeti ya Leo Machi 28,2023

March 28, 2023
WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA

WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA

March 28, 2023
SAKA AIBUKA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI EPL

SAKA AIBUKA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI EPL

March 31, 2023
HOMA YA DENGUE YAIBUKA KWA KASI SUDAN

HOMA YA DENGUE YAIBUKA KWA KASI SUDAN

March 31, 2023
NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, wateja kuzoa Mil. 180/-

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, wateja kuzoa Mil. 180/-

March 31, 2023

Mtanzania aibuka kinara tuzo za uvumbuzi kwenye teknolojia barani Africa

March 31, 2023
Facebook Twitter Google+ Youtube RSS

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

No Result
View All Result
  • Home
  • HABARI
  • BIASHARA
  • Lifestyle
  • BURUDANI
  • MICHEZO

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In