Na Khatimu Naheka
MUDA mfupi baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Kocha wa Yanga, Ernie Brandts ameliambia gazeti hili kuwa, anaondoka kuelekea kwao Uholanzi lakini hajasaini mkataba mpya Yanga.
Akizungumza na Championi Ijumaa muda mfupi baada ya mchezo dhidi ya JKT Oljoro uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Brandts alisema amelazimika kuondoka haraka kuiwahi familia yake ili kuweka mambo sawa kuhusu familia yake.
โNaondoka muda mfupi kutoka sasa (jana usiku), narudi nyumbani mara moja, kuna mambo natakiwa kwenda kuyafanya kule, kuhusu kusaini bado sijafanya hivyo, nafikiri tusubiri kwa sababu sijajua mpango wa viongozi wa klabu,โ alisema Brandts.
Aidha, kocha huyo amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo baada ya kusema atarudi nchini mapema kwa lengo la maandalizi ya kikosi chake hicho kitakachoanza majukumu ya mechi za Klabu Bingwa Afrika mapema mwakani.
CHANZO; GPL
Tuliishi maisha ya shida sana kisa uchawi wa jirani!
Kwa hakika uchawi na mambo ya kishirikina huwa yamesimika mizizi katika sehemu nyingi za Afrika, jina langu ni Julius, nilililewa...
Read more