
www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA Karama Nyilawila amewataka mabondia wa Tanzania kuacha imani za kishirikina na badala yake wafanye mazoezi ili waweze kufikia mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyilawila alisema hapendezwi na vitendo hivyo kwani vinauwa viwango vya michezo nchini. Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi.
Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika mazoezi makali chini ya meneja wake Seleman Zugo na kwamba amejipanga kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa K,O ya raundi ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila ‘Super D’ uliofanyika NOVEMBA 10 katika ukumbi wa Zulu Paradise pugu kilumba