![]() |
Mashabiki wa Simba |
Matokeo ya mchezo la ligi kuu ya Voda Com si Simba wala Mbeya City baada ya timu hizo zote mbili kutoka uwanjani hapo kwa kifua mbele cha goli 1-1.
Mchezo huo ambao kwa Mbeya City ni mchezo wa nyumbani imeweza kuonyesha umakini mkubwa wa kugomea kufungwa katika uwanja wa Nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya huku Simba nayo ikikwepa ” kugagaduliwa ” ugenini kiasi cha kuifanya Simba kukomaa na kusawazisha goli la Mbeya City lililofungwa kipindi cha kwanza huku Simba ikisawazisha goli hilo kipindi cha pili .
Timu ya Mbeya City ambayo awali iliweza kufanya vema kwa Yanga kulazimisha sare pia leo imeweza kulazimishwa na Simba kutoa sare ya goli 1-1
Wakati huo huo timu ya Lipuli Fc Iringa imefanikiwa kuichapa timu ya Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi daraja la kwanza mzunguko wa pili kwa jumla ya goli 3-1
Mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Samora mjini Iringa huku wadau wa soko wakiipongeza kwa mchezo huo.