Robyn Rihanna Fenty, maarufu sana kama Rihanna ni mwanamuziki na mwigizaji mkali na hapo hakuna ubishi. Mbali na kipaji, huyu mdada pia ni mrembo wa nguvu mwenye mvuto lakini zaidi ana vioja au vituko vya kutosha hasa linapokuja suala zima la uvaaji. Rihanna anaonekana kupenda sana hewa hapendi kufunika sana mwili wake unaotoa udenda wanaume wengi. Anapenda sana mavazi ambayo bongo tunaita nusu-uchi, lakini wakati mwingine anaweza kuvaa bikini peke yake na kuanzia tumboni kwenda juu asivae kitu chochote. Wakati mwingine hufanya kwa ajili ya majarida ya biashara ambazo zinamwingizia mkwanja mrefu lakini Rihanna anavuka mipaka.
Instagram, mtandao wa kijamii wa kushare picha na vidio uliondoa picha ya Rihana inayoonekana kwenye picha juu, Rihana alipost picha hiyo akiwa hajavaa kitu chochote kuanzia tumboni hadi kifuani Jumanne iliyopita na saa 1 baadaye Instagram waliiondoa picha hiyo ambayo inavunja sheria za uvaaji.
Chanzo kutoka Instagram kiliiambia TMZ kuwa Rihanna alitumiwa meseji na Instagram kama onyo kuwa aweke picha za heshima au vinginevyo wataifungia akaunti yake.
Lakini “kama bikini inavyojaribu kuyazuia makalio” Instagram haikufanikiwa kumzuia mlimbwende huyo kwani ameendelea kupost picha za aina ileile katika mtandao wa Twitter. Zikodolee hapa