Tukio ambalo limemalizika usiku wa kuamkia leo ndio talk of the town kama wasemavavyo watasha hapa jijini Dar, Tanzania na hata Afrika nzima.Tukio hilo ni KTMA, tunzo kubwa zaidi za muziki nchini Tanzania.Matukio mengi madogomadogo ndani ya tukio hilo kubwa yamejitokeza, kubwa la kihistoria ni la Diamond Platnum kubeba tunzo zote alizokuwa akiziwania. Diamond amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na 20% ya kuchukua tunzo tano kwa mwaka mmoja kwani yeye ameweza kuchukua tunzo saba.
Tukio jingine la kusisimua ni kitendo cha mwanahip-hop Fid Q kubeba tunzo mbili jambo ambalo lilikata kiu ya muda mrefu ya mashabiki wake. Pia Christian Bela alichukua tunzo kwa mara ya kwanza katika tasnia ya muziki wa dansi. Show za wasanii kama Mwana FA, Vanesa Mdee na Makomando pia zilikua gumzo.
Mbali na matukio ya jukwaa kuu kulikua na tukio la mahojiano lililoandaliwa na timu ya KTMA ambapo kila msanii alikuwa akihaojiwa baada ya kuchukua tunzo. Kitengo hiki kilisimamiwa na watangazaji maarufu kama Millard Ayo, Jokate na Samy Sago. Baada ya Diamond kunyakua tunzo yake ya saba mrembo wake Wema Sepetu alishindwa kuficha furaha yake kwani aliamua kuambatana na Dangote katika kufanyiwa mahojiano. Hapo Wema hakutaka kuficha kitu kwani alianza kwa kusema”tumezichukua tunzo zote na hakuna swali katika hilo” na katika kuonesha kuwa wako katika ulimwengu wa “mahaba niue” Wema aliamua kusema “Naomba Watanzania watambue ya kwamba mimi(Wema) na Diamond ni wapenzi”. Tukio lingine la hivi karibuni ambalo limedhihirisha mahaba ya wmasupastaa ha ni shoo yao ya “Heels&Ties” iliyofanyika Mtwara May 2 Ijumaa iliyopita.
Matukio haya yanachanganya vichwa vya mashabiki wa masupastaa hawa kwani sio muda mwingi umepita Wema na Diamond walizinguana na kutemeana mbovu kwenye vyombo vya habari. Na hii inafanya tunajiuliza je ni drama tu au kweli ni mahaba niue?
NMB ya kwanza kuzindua Malipo kwa QR na UnionPay International
NA MWANDISHI WETU BENKI ya NMB kwa kushirikiana na UnionPay International (UPI), wamezindua suluhisho la malipo ya kimtandao kupitia QR...
Read more