
Furaha ya kiungo wa mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Mfaransa Samir Nasri imepukutika ghafla baada ya kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps kutangaza kikosi kitakachoshiriki kombe la Dunia Brazil bila kutaja jina la kiungo huyo wa Manchester City. Kiungo huyo ambaye amekuwa katika fomu nzuri na ambaye alifunga goli la kwanza katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza amesema maneno haya kueleza hisia zake “Nayaheshimu maamuzi ya kocha, na nitalitazama kombe la Dunia kwenye TV” aliongeza “Kama kuanza katika kikosi cha Man City na kushinda makombe mawili kwa msimu haitoshi, basi sijutii chochote”
Wachezaji wengine ambao wameachwa kwenye kikosi cha Didier Deschamps ni Eric Abidal,na Gael Clich. Samir Nasri hayupo hata katika orodha ya wachezaji saba wanaotarajiwa kuongezwa katika kikosi hicho cha ufaransa.
Hii ndio orodha ya kikosi cha Ufaransa
Magolikipa: Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Olympique Marseille), Mickael Landreau (Bastia)
Walinzi: Mathieu Debuchy (Newcastle United), Lucas Digne (Paris St Germain) Patrice Evra (Manchester United), Laurent Koscielny (Arsenal), Eliaquim Mangala (Porto), Bacary Sagna (Arsenal), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real Madrid)
Viungo: Yohan Cabaye (Paris St Germain), Clement Grenier (Olympique Lyon), Blaise Matuidi (Paris St Germain), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba (Juventus), Moussa Sissoko (Newcastle United), Mathieu Valbuena (Olympique Marseille)
Washambuliaji: Karim Benzema (Real Madrid), Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (Newcaste United), Franck Ribery (Bayern Munich)