Ni habari rahisi sana kusoma au kusikia lakini sio rahisi kuingia akilini kuwa supastaa Justin Bieber anashutumiwa kufanya kitendo cha ukabaji, tena akifanya kitendo hicho cha kujaribu kupora simu ya mkononi ya mwanamke. Kitengo cha Polisi huko Los Angeles kimethibitisha kupokea tuhuma hizo kutoka kwa watu kikundi cha watu waliokuwa Sherman Oaks Castle Park na wanazifanyia uchunguzi. Watu hao wanadai kuwa Bieber alifanya tukio hilo mahali hapo siku ya Jumatatu, alipoamua kumfanyia ubabe mwanamke huyo kwa tuhuma za kumpiga picha, ingawa mwanamke huyo hakuhusika na suala la upigaji picha.
Mwanamke huyo amesema kwamba Bieber alimtuhumu kwa kumpiga picha kitendo ambacho sio cha kweli, na Bieber alimvamia mwanamke huyo ambaye alikuwa na bimti yake wa miaka 13 na kuichukua simu kwa nguvu katika mkoba wa mwanamke huyo. Mwanamke huyo amesema baada ya Bieber kushindwa kutoa lock ya simu hiyo alimrudishia simu yake na yeye kumuonesha kuwa hakuna picha yoyote aliyompiga isipokuwa yeye na binti yake walitakaka kusalimiana naye tu.
Bieber alitoa maneno ya kejeli kwa mwanamke huyo akisema “unajidhalilisha mwenyewe mbele ya binti yako, kwani huwezi kuwa mbali na hapa?
Mwanamke huyo ameshajaza waraka wa malalamiko na Polisi wanafanya uchunguzi ili kujua kama mkali huyo wa Confident amevunja sheria.