Hii ni kama zawadi kwa kiwango kizuri walichokionesha Mbeya City Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Wakiwa mamepanda daraja Mbeya City ilibuka kuwa tishio katika msimu wa ligi uliomalizika na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ikitanguliwa na Yanga na mabingwa Azam FC, Mbeya City wameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano hiyo itakayofanyika Sudani kuanzia Mei 22.
Afisa habari wa CECAFA Rodgers Mulindwa aliuambia mtandao wa Goal kuwa timu nyingine kubwa zitakazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Al Masry ya Misri, El Merreikh na Al Ahli.
Mulindwa aliongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika katika miji kama Khartoum, Sandy na Red Sea-side na Eritrea peke yake ndio bado haijathibitisha ushiriki katika michuano hiyo.
Mbeya City wako katika kundi B lenye timu kama El Merreikh Al Fasher ya Sudan, Elma ya Somalia na AFC Leopards ya Kenya.
Timu kutoka Tanzania Visiwani, Polisi Zanzibar FC ipo katika kundi A pamoja na timu kama El Merreikh ya Sudan,SC Vitoria University ya Uganda, na Malakia ya Sudan Kaskazini.
Kundi C lina timu kama Al Ahli Shandi ya Sudan, Al Masry ya Misri, Defence ya Ethiopia na Dikhil ya Djibouti
Kundi D lina timu hizi hapa, Hey Al Arab ya Sudan,Arab Contractors ya Misri,Flambeau de I’Eist ya Burundi na Etincelles ya Rwanda.
Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atanyakua kitita cha dola za Kimarekani 30, 000, mshindi wa pili 20,000 na wa tatu 10,000.
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias akishuhudia mteja Dosian Augustine akifanya muamala katika...
Read more