Ni kitendo cha kustaajabisha,lakini ndio kimeshatokea. Tukio hili kama linavyoonekana katika video limetokea jana Ijumaa katika sherehe za Cannes Film, ambazo zilianza Jumatano, May 14 na zitaendelea hadi May 27. Mwandishi wa habari anayefahamika kama Vitalii Sediuk ndiye aliyemharibia siku mwanadada America Fereira baada ya kulala chini na kuzama ndani ya gauni refu alilokuwa amevaa mwigizaji huyo kwa lengo la kumchungulia.
Mwandishi huyo ambaye amezinasa picha za mastaa mbalimbali katika hafla hiyo kwa ufundi wake wa kupiga picha, alizua zogo la ghafla katika Red Carpet hiyo ya onesho la How to Train Your Dragon 2 baada ya kufanya kitendo hicho kwa mwigizaji huyo.
Mbali na kufanyiwa kitendo hicho Fereira pamoja na mastaa wenzake walibaki katika hali ya utulivu na kuwaacha watu wa usalama ambao walimtoa Sediuk katika eneo hilo.
TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO:
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias akishuhudia mteja Dosian Augustine akifanya muamala katika...
Read more