Wadau wengi wa muziki huwa wanamkosoa mkali Justine Bieber kwa vitendo vyake vya ukorofi na mara nyingi supastaa Bieber amekuwa akifanya vitu ambavyo huwaacha mashabiki wake midomi wazi.
Usiku wa jana Bieber aliendeleza vituko vyake baada ya kupanda jukwaani katika club ya Gotha Club iliyopo huko Cannes na kuanza kumsapoti Rick Ross aliyekuwa akitumbuiza katika club hiyo.
Justin Bieber hakuishia hapo kwani alikamata kipaza n kuanza kuchana wimbo wa Tupac, Dear Mama.
Haya ndo maisha ya kisela ambayo Justin Bieber ameyachagua na anayapenda ingawa wadau wengi wa muziki wanakandia kuwa maisha hayo hayampendezei. Si mara ya kwanza Bieber kupanda jukwaani na kurap kwani pia aliwahi kurap wimbo wa Otis.
Itazame video ya Bieber akifanya tukio hilo.
NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, wateja kuzoa Mil. 180/-
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paul Chacha pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya...
Read more