Na Mayasa Mrisho
MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuondokewa na Adam Kuambana ni pigo kubwa kwa tasnia ya filamu lakini zaidi pengo lake linajidhihirisha katika eneo la madairekta.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akisoma wasifu wa Adam Phillip Kuambiana.
Akizungumza na paparazi wetu, Steve alisema katika tasnia ya filamu nchini, madairekta wazuri ni wachache sana hivyo Kuambiana alikuwa kama tegemeo la wengi na kifo chake ni pigo sana eneo hilo.

“Tulikuwa tunategemea mengi zaidi kutoka kwake, madairekta wengi walikuwa wakimtazama yeye hivyo kimsingi tuombe sana Mungu atujalie tupate vipaji vingine vitakavyoweza kuziba pengo lake,” alisema Steve.
GPL