Staa wa ngoma kali ya Loyal ameawekwa huri rasmi leo baada ya kuishi takribani miezi mitatu gerezani. Breezy alihukumiwa gerezani kwa siku 131 baada ya kukiuka masharti ya kifungo huru ambacho alihukumiwa baada ya kumchapa makonde aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, supastaa Rihana.
Hata hivyo kuachiwa kwa Chris ni kwa muda tu kwani ana kesi nyingine ya kujibu, baada ya kumfanyia fujo shabiki mmoja huko Washington DC. Na kama atapatikana na hatia katika kesi hii itambidi aendelee kunyea ndoo kwa miezi 6 tena.
Mara tu baada ya kuachiwa huru msanii huyo ambaye ni mmoja ya wasanii wanaowania tunzo za BET alitweet maneno ya kumshukuru Mungu na kuonesha kuwa amerudi katika tasnia ya muziki.
Equity Bank, ZEEA, na SMIDA wasaini Makubaliano ya Ushirikiano wa Kutoa Mikopo Nafuu Tanzania
Mkurugenzi wa ZEEA Mh. Juma Burhani,mkurugenzi wa SMIDA Mh. Soud Said Ali na mkurugenzi mtendaji wa Equity bank (T)...
Read more