
Jembe la kazi: Luis Suarez alikuwa nyota wa Mchezo Italia ikiifunga England mjini Sao Paulo.

Suarez, ambaye alikosa mechi ya ufunguzi ya Uruguay akishangilia bao la kwanza Sao Paulo.
LUIS Suarez amekiri kuwa magoli yake mawili ambayo yamewaacha England njia panda katika fainali za kombe la dunia ni kisasi kitamu kutokana na ukosoaji waliofanya juu yake wakati anacheza ligi kuu ya nchi hiyo.
Nyota huyo wa Uruguay na Liverpool alifungiwa kwa kumfanyia ubaguzi wa rangi beki wa kushoto wa Ufaransa na Manchester United, Patrice Evra. Pia kitendo chake cha kumung`ata kwa meno beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic kilimufanya afungiwe katika msimu wa utata kwake nchini England.
Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya England, Suarez, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji wa goti alisema: “Niliota jambo hili, Nafurahia muda huu, kwasababu ya yote niliyoumia, ukosoaji niliopokea. Kwahiyo, mnaondoko.”