MASHABIKI wa sinema za Kibongo wamefunguka kuwa wanapenda uhusiano waliouita wa kimapenzi kati ya Wakurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’.
Ishu hiyo ilijidhihirisha wazi juzikati mjini Dodoma wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wamekwenda kuzindua video ya wimbo wa Tuulinde Utanzania katika Uwanja wa Jamhuri.
Mashabiki walidai wanapenda kuwaona wawili hao wakiwa pamoja ingawa wenyewe wamekuwa wakikanusha kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi zaidi ya kazi.
“Tunapenda kuona Johari na Ray wapenzi maana ni watoto wa mji wa Dodoma na tunawakubali sana,” alisema shabiki mmoja aliyetambulisha kwa jina la Ally.
CHANZO; GPL