KOCHA wa Colombia, Jose Pekerman anatarajia kuwaona Brazil wakiwa katika kiwango chao bora kuelekea katika mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia utakaopigwa kuanzia majira ya saa 5 usiku wa leo.
The Selecao wamekuwa wakikosolewa na vyombo vya habari vya nchini mwao kwa kiwango chao `mbofu mbofu` katika mashindano ya mwaka huu, hususani baada ya kupata ushindi wa kubahatisha wa mikwaju ya penati dhidi ya Chile hatua ya 16.
Pekerman hatarajia kuwaona wenyeji wakiwa na presha baada ya mchezo wa Fortaleza dhidi ya Chile.
“Kufuzu nusu fainali ni matarajio makubwa na kila timu itacheza kwa kiwango chake cha juu ili kupata nafasi hiyo”.
CHANZO; FULL SHANGWE