Baada ya kuwa na tetesi katika mtandao wa kijamii wa Twitter juu ya Drake kutokutumbuiza katika show mblili ya London na Birmingham katika tamasha la Wireless Festival huko nchini Uingereza, kitu ambacho ni kinyume na matarajio, waandaaji wameweka wazi kuwa ni kweli.
Rapa huyo kutoka kundi la Young Money ambaye anashikilia tunzo ya BET ya mwanahiphop bora 2014 amepata matatizo ya kiafya na kwa mujibu wa maelekezo ya daktari; Drake hatakiwi kusafiri kwa ndege wala kufanya shughuli yoyote ya kutumia nguvu mpaka hali yake itakapotengamaa.
Mkali mwenzake Kanye West ndiye amepewa jukumu la kumkaimu Drake na leo Kanye West ataanza kupiga mzigo pale Finsbury Park jijini London na kesho tarehe 5 atamalizia kule Birmingham.
Hiki ndio amekisema Drake kudhihirisha upendo wake kwa mashabiki:
“To my beloved fans, it truly breaks my heart that I won’t be able to perform as planned at Wireless and Roskilde this weekend. I got stick a few days ago and although I am on my way to bouncing back, my doctors have made it clear that I am not physically fit to fly or deliver the performance my fans expect and deserve from me. I will be focused on resting for a quick recovery. I have the best fans in the world and I can’t wait to come back to make more incredible memories together”
HARAKATI360 inamwombea Drake apone mapema.