Mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba ametangaza rasmi leo kuachana na soka la kimataifa, kwa maana kwamba ametundika daluga rasmi kwa timu yake ya taifa ya Ivory Cost. Drogba ambaye ameichezea Ivory Cost jumla ya michezo 104 na kufunga magoli 65, pia amekuwa nahodha wa timu hiyo kwa miaka 8 na kulitumikia taifa lake miaka 12.
Drgba amerejea katika timu ambayo ilimtengenezea jina zaidi, Chelsea na kusaini mkataba wa mwaka mmoja huku akiikacha Galatasaray.
Akizungumzia uamuzi wake wa kustaafu timu ya taifa, Drogba mwenye umri wa miaka 36 amesema “Ninajihisi fahari kuwa nahodha wa timu yangu ya taifa kwa miaka 8 na kuiweka nchi yangu katika ngazi ya Dunia katika soka”.
Baada ya kufukuzwa kazi mume naye kanikimbia ila….!
Tuliishi pamoja na mume wangu Kibet katika kaunti ya Lamu ambapo nilifanya kazi ya udaktari katika hospitali moja ya kibinafsi...
Read more