…t.

Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba bilionea mmoja hakupendezwa kumuona mwakilishi wao Tayo akiambulia patupu, bilionea huyo Ayiri Emami amempatia Tayo Folarin pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango ambacho kimetolewa na BBAHotshots kwa mshindi wa kwanza.
Tunawafahamu mabilionea wachache kutoka Nigeria wakiongozwa na Aliko Dangote,Emami leo anakaa kwenye headlines karibu zote za Nigeria kwa kumpatia Tayo dola laki tatu na nusu (350,000/=).
Kiasi hicho ni backup kwa Tayo ambaye alionekana mnyonge sana usiku ambao Idris alitangazwa mshindi, hii itampa Amani ya kuendelea maisha na mpenzi wake na mtoto wake mmoja ambaye alizaliwa wakati Tayo akiwa ndani ya Jumba la Big Brother.