Mkali na mkongwe wa R&B, Usher Rymond ameamua kwa mara nyingine kujitoa katika soko la ukapera baada ya kumvisha pete ya uchumba Grace Miguel ambaye ni mpenzi wake kwa muda mrefu.
LoveBScott limepasha habari kuwa wawili hao wako kwenye mipango ya harusi na punde si punde watakuwa mume na mke.
Usher na Grace hawajazungumza chochote lakini kwa upande wa Usher amekuwa akificha sana mahusiano yake na Grace mpaka pale alipohojiwa na Billboard siku za karibuni na kusema:
“Nina mwenza na meneja wa kipekee sana. Amenisaidia sana katika nyakati ngumu za maisha na kazi yangu ya muziki”
Tunamtakia kila la kheri Usher na Grace katika mahusiano yao.
CALISAH ATAKA ALIPWE LAKI 3 NA NUSU KUJIBU DM
Mwanamitindo (model) maarufu Afrika kwa sasa Kalisa Abdul (@calisah) amejigamba kuwa ni miongoni mwa watu wenye DM nyingi zaidi za...
Read more