Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu amekataa kuwa amerudiana na mpenzi wake wa zamani Chaz Baba japo amedai kuwa muimbaji huyo wa muziki wa band ndiye mwanaume wa pekee ambaye hakuwa na masuala ya kiswazi baada ya kuachana.
Wema ameiambia U Heard ya Clouds FM Jumatano hii kuwa Chaz Baba kwa sasa ni mshkaji wake na hata alipooa alimchangia pesa.
“Chaz Baba alikuwa ni msikaji wangu naweza kusema ndio boyfriend pekee asiye na mambo ya Kiswahili,” amesema. “Tulizinguana tukafika pointi tukasaidiana, ameoa nikamtolea mchango, nimeenda kwenye harusi yake sioni tatizo.”
“Mimi na Chaz Baba tulikuwa tunapendana na baada ya kufikia point ya kuachana tukaachana, tukawa hatuongei for sometime mwisho wa siku baada ya kila mmoja kukaa kwake tukawa tunazungumza. Sio kama watu wengine tukigombanaga tunatafuta mabifu, hatusemeshani,” alisema mrembo huyo na kusisitiza kwasasa hana bwana …‘sina bwana’ alisema.
BENKI YA CRDB KATIKA MAONESHO YA 46 YA SABASABA
Mgeni Rasmi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya...
Read more