Video ya rapa Joh Makini kutoka kundi la Weusi, aliyomshirikisha rapper wa Afrika kusini, Aka ‘Don’t bother itatambulishwa rasmi na kwa mara ya kwanza leo [Nov. 10] kupitia kituo cha runnga cha MTV Base.
Video hiyo itaoneshwa saa 12 za jioni (Masaa ya Afrika Mashariki) kwa mara ya kwanza kwenye kituo icho.
Wimbo huo umerekodiwa chini ya studio za The Industry chini ya producer Nahreel na video imerekodiwa Afrika kusini chini ya director Justin campos.