MSANII anayefanya poa kwenye ulimwengu wa muziki Bongo, Moshi Katemi ‘Mo Music’ jana aliandaa hafla fupi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa (birthday) iliyofanyika maeneo ya Sinza- Palestina jijini Dar.
Mbali na kusherehekea birthday yake hiyo, Mo Music pia aliachia ngoma yake mpya kama zawadi aliyoipa jina la Skendo ambayo imeonekana kupokelewa kwa kishindo na mashabiki.