







MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Zambia, Robert Chindaba Banda ‘Amarula’, kesho anatarajiwa kukamua kwenye Ufukwe wa Escape One Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Freconic Ideaz waandaaji wa onesho hilo, Fred Ngimba, amesema baada ya kufanyika Escape One kesho, litafanyika Ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma.
Naye msanii huyo aliyeambatana na kundi lake alisema katika maonesho hayo atahakikisha anaonesha makali yake na kuacha gumzo hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Onesho hilo linatarajiwa kusindikizwa na wasanii wa muziki kizazi kipya hapa nchini wakiwemo Benpol, Roma Mkatoliki, Fred Swag, Msouth na wengineo.
PICHA: RICHARD BUKOS / GPL