Rufaa iliyowasilishwa kwa kamati ya nidhamu ya FIFA na aliyekuwa rais wa shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini imetupiliwa mbali.
Hata hivyo kipindi cha marufuku ya wawili hao imepunguzwa hadi miaka 6.
Maafisa wawili wakuu zaidi katika usimamizi wa kandanda duniani walikuwa wamepigwa marufuku ya miaka 8 ya kutoshiriki kwa vyovyote maswala ya soka kufuatia uchunguzi wa kimaadili dhidi yao.
Walipatikana na hatia ya ukiukaji wa maswala mbalimbali kama vile kashfa ya dola milioni 2 malipo yasiyo rasmi ambazo zilikabidhiwa Platini mwaka 2011.
Maafisa hao wawili wanasisitiza hawakufanya makosa yoyote.
Sasa wawili hao wameapa kukata rufaa tena katika mahakama kuu ya michezo (Court of Arbitration for Sport)
Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 amesema kuwa hajaridhiashwa kabisa na kamati hiyo ya rufaa ya FIFA.
Platini kwa upande wake amesema hilo ni tusi kwake.
Uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo utafanyika ijumaa huko Zurich Uswisi.