Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akipeana mkono na Mmoja wa wanafunzi waliopata udhamini wa tigo Carolyne Paul, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Udsm shahada ya uhandisi wa kompyuta na teknolojia ya habari wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo jijini Dar Es Salaam.
|
Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez(katikati) akipata “SELFIE” na ,Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula na Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua mafunzo ya Tehama mara baada ya kampuni ya Tigo kutangaza udhamini wa jumla ya shilingi million 300 kwa wanachuo hao mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam . |
Dar es Salaam Machi 23, 2016 Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo wametangaza kudhamini wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa kwa jumla ya shilingi million 310.
Akitangaza udhamini huo jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema fedha hizo zitagharamia ada ya chuo, gharama za kufanya utafiti, malazi na chakula kwa kipindi cha miaka minne cha masomo ya Tehama kwa kila mwanafunzi.
Gutierrez amesema udhamini huo unaowalenga kuwasiadia vijana wenye vipaji katika taaluma ya Tehama kutimiza ndoto zao za kimaisha ni sehemu ya sera ya kampuni hiyo ya mawasiliano ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kukuza sekta ya tehama na kuleta maendeleo nchini.
“Tunaamini kupitia udhamini huu kampuni yetu, kwa kushirikiana na DTBi, inatoa mchango wake katika kujenga kizazi kijacho cha mabingwa katika sekta ya Tehama ambao watakuwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi hii,”Gutierrez amesema akiongeza kwamba tayari kuna makubaliano kati ya Tigo na DTBi unaowapa wanafunzi kutoka DTBi fursa ya kubuni bidhaa mbalimbali vya Tehama ambavyo hutumiwa na Tigo kibiashara na mapato kugawanywa kwa wadau wote.
Wanafunzi tisa waliobahatika kupata udhamini wa Tigo ni Erickson Muyungi (UDSM), Fatma Moshi (UDSM), Caroline Paul (UDSM), Michael Lunyungu (UDOM), Robert Charles (UDOM), Isack Kipako (UDOM), Jacqueline Dismas (UDSM), Jumanne R. Mtambalike (IFM) na Joel Mtebe (UDSM).
Akizingumzia zaidi kuhusu mkataba huo kati ya Tigo na DTBi, Mkurugenzi huyo wa Tigo amesema: “mbali na udhamini tunaoutoa kwa wanafunzi wa Tehama tuna mradi wa pamoja uitwao ‘Project Digitize’ ambao umewawezesha wanaTehama chipukizi kuanzisha kampuni zao kuipitia ubunifu wao na ambao wanapata msaada kutoka Tigo katika kuendeleza miradi yao. Hadi leo kuna wanatehama watatu wanaosaidiwa na Tigo kupitia mpango na ambao bidhaa pindi bidhaa zao zitakapoanza kutumika kibiashara, watafaidika kutokana na mgawanyo wa mapato..”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi Mhandisi George Mulamula kwa upande wake amesema üshirikiano na Tigo umetoa fursa na njia za kibunifu kwa wanafunzi wa DTBi kupata elimu, kujenga uwezo wao wa Tehama ambavyo vitawasaidia kuonyesha vipaji vyao katika fani hii ndani na nje ya nchi.”
Mulamula aliongeza kusema kwamba: “DTBi’s ina malengo ya kuwahamasisha vijana wakiwemo wanawake kujenga tabia za kuwa wajasiriamali Tehama ili kusaidia kukuza sekta binafsi na kuongeza makusanyo ya kodi nchini. Katika kutekeleza azma hii, Tigo imetoa mchango mkubwa kwa kuwawezesha wajasiriamali wetu kufikia ndoto zao za uzalishaji mali, kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, kuleta nafasi mpya za ajira yote haya yakiwa ni vielelezo vya jinsi ambavyo tehama inaweza kusaidia kukuza pato la taifa.”