|
Kutoka kushoto ni Emmanuel Buttorn, Rose Minja (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto) na Christopher Mushi wote kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. . |
Mratibu wa kipindi cha Walinde watoto Neema Kimaro na Kimela Billa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto wakizungumza na waandishi wa habari.katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. |
Tabu Salum kutoka redio ya Sauti ya Quran akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. |
Waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto wakijadiliana mara baada ya mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. |
Mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu Ukatili kwa watoto
Tatizo la Ukatili dhidi ya watoto, linaongezeka siku hadi siku, na kuleta athari mbalimbali za kimwili, kiakili, (kisaikologia) na kiafya kwa watoto. Watoto wanaumizwa, kubakwa, kunajisiwa, kutelekezwa, kusafirishwa kibiashara na kufanyishwa kazi za hatari zinazoathiri afya zao. Matendo haya ya kikatili hayakubaliki kabisa.
Yafuatayo ni mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu ukatili kwa watoto:
1. Aina za ukatili
Ukatili dhidi ya watoto upo wa aina nyingi. Ukatili wa Kijinsia, ni vitendo au maneno yanayoweza kusababisha madhara kwa mtu au kundi la watu kutokana na maumbile yao. (Mf: kuguswa bila ridhaa, jaribio la kubaka/kubaka, kulazimisha kufanya ngono n.k). Ukatili wa Kimwili ni kama kupigwa, kusukumwa, au kutishiwa kuuwawa kwa silaha. (Mf: kuonyeshwa kwamba hutakiwi, vipigo vya mara kwa mara) na Ukatili wa Kiakili/Kisaikolojia, kutelekezwa, kubaguliwa, kutishwa. (Mf: kuitwa majina mabaya, kunyimwa huduma za msingi, kufanyishwa kazi ngumu n.k)
2. Wahusika wa Ukatili dhidi ya watoto
Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania ulifanyika mwaka 2009 na uliongozwa na Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta mbalimbali za Serikali, Asasi za Kiraia na Wadau wa Maendeleo. Katika utafiti huo ilionekana kuwa ndugu wa karibu kama mjomba, baba, walezi na walimu ndio wanaosababisha ukatili dhidi ya watoto. Kwa kuona hivyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wakaona umuhimu wa kuanzisha mpango wa kuelimisha jamii kuzuia ukatili dhidi ya watoto.
3. Nini kifanyike kupunguza ukatili kwa watoto
Wananchi wote kwa ujumla wana jukumu la kuhakikisha kwamba wanawalinda watoto. Wazazi / walezi wanapaswa kujua watoto wao walipo na wanachokifanya kila wakati na kuhakikisha usalama wa mahali watoto wanapopenda kutembea mara kwa mara. Watoto wapewe moyo kuripoti vitendo mbalimbali vya ukatili.
4. Umuhimu wa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto – namba 116
Kituo cha huduma ya simu kwa mtoto ni muhimu katika mifumo ya ulinzi wa mtoto nchini. Ni sehemu pekee ambayo mtoto au Mzazi/Mlezi anaweza kupiga simu na kutoa taarifa za ukatili kwa siri na kupata huduma ya ushauri nasaha na rufaa kwa msaada zaidi kwa mujibu wa tatizo lolote linalohusu ukatili dhidi ya watoto. PIGA SIMU BURE kwenda namba 116 kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto.
5. Uchumi na Familia
Familia zikiwa na hali ngumu ya kiuchumi husababisha ugomvi kati ya wanafamilia na hii huweza kupelekea kutelekezwa kwa watoto au kuwatenga watoto na familia, jambo ambalo litaongeza hatari ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. Vilevile ugumu wa maisha ni kisababishi cha watoto wanaofanya kazi katika umri mdogo, kuchuuza /kufanya biashara ya watoto, mimba zisizotarajiwa na ndoa za utotoni. Hivyo basi ni muhimu wazazi/walezi kujishughulisha na kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama wa vikundi ili waweze kuzalisha mapato ya kusaidia mahitaji ya familia.
6. Madhara ya adhabu kwa watoto
Kuna madhara mengi sana ambayo yanaweza kuwapata watoto kutokana na kupewa adhabu mbalimbali. Adhabu huleta hasira na chuki ambayo haisaidii kuleta mabadiliko ya tabia. Kadri adhabu inapokuwa kali zaidi ndivyo inavyopelekea mtoto kuwa na matatizo ya kutojithamini, kuwa mhalifu, kupata magonjwa ya akili na kuwa na tabia ya ukatili. Adhabu mara nyingi haitoi mchango chanya kwa maendeleo ya mtoto
7. Ishara ambazo huonyeshwa na watoto waliofanyiwa ukatili
Ni muhimu kwa wazazi/ walezi kutambua ishara mbalimbali zinazoonyeshwa na mtoto aliyefanyiwa ukatili. Ishara hizo ni kama vile mtoto kutojiamini hata kama anafanya kitu sahihi anakua na hofu kwa sababu tu anahisi anaweza kupigwa. Mtoto kukataa kwenda sehemu ambazo amezoea mf. shule, ukifuatilia kwa ukaribu utakuta kuna mtu anamfanyia ukatili huko au njiani.
8. Wasikilize kwa makini
Ni muhimu kujijengea mazingira ya kumsikiliza mtoto kwa makini. Unapofanya hivyo ni muhimu ajue kuwa unamsikiliza, aidha kwa kutumia ishara bila maneno; kama vile kuashiria kwa kichwa. Mtazame mara kwa mara kwa mtazamo wa kirafiki. Unaweza pia kurudia aliyokwambia kwa maneno mengine.
9. Umuhimu wa vyombo vya habari kupambana na ukatili
Kwa mujibu wa mwongozo wa vyombo vya habari wa kuandika habari za watoto uliochapishwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), “Watoto wanahitaji uangalizi maalum wa kuwajali na kuwalinda. Wakati wa kuandika habari za watoto, vyombo vya habari vinapaswa kujenga taswira sahihi kwa watoto ili kuwaepusha katika hatari ya kuadhibiwa au kunyanyapaliwa. Watoto ni binadamu wanaohitaji kutambuliwa, kupewa hadhi, utu, heshima na zaidi ya yote kulindwa. Kutokana na ukweli huo, uelewa, umakini na weledi wa uandishi wa habari zinazowahusu wao kwa kuzingatia hali yao na mahitaji yao ni muhimu. Kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kuboresha uandikaji wa habari za watoto na wakati huo huo kulinda usalama wao kimwili na kihisia/jaziba. “
Mambo haya yameibuka katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro.
Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
Redio hizo ni pamoja na Kitulo FM, Radio Maria, Radio Faraja, Boma Hai Radio, Uplands FM, Radio Sauti ya Quran, Kwizera FM na Country FM.
Nyingine ni Bomba FM, Zenji FM, ZBC, Radio Huruma, Ice FM, Radio Jamii Kilosa, TBC Taifa, Dodoma FM, Fadeco Radio, Radio Victoria na Best FM.
Waandishi wa habari wametakiwa kushirikiana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa haki za watoto zinatekelezwa hapa nchini.
Ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kuwa anawalinda watoto na kuwasadia kukua na kufikia ndoto zao katika jamii.