![]() |
Semina ya unywaji kistaarabu ikiendelea |
![]() |
Askari wa usalama barabarani wakisikiliza kwa makini |
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Arusha Mhandisi Nuru Kacharia Seleman, amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Mhandisi Seleman.
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Bi Mhandisi Seleman.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia Mhandisi Seleman anasema “ama kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.