Hatma ya muda mrefu ya mlinzi wa RB Leipzig Dayot Upamecano inaonekana kutokuwa na uhakika kuendelea kusalia klubuni hapo baada ya kuwaniwa na magwiji wa Ligi kuu ya Uingereza.
The Mail Jumapili imeripoti kwamba Chelsea wamejiunga na orodha ya vilabu vinavyomuwania Upamecano, wakiwa katika ushindani dhidi ya Manchester united iliyoonesha kuvutiwa zaidi na beki huyo kwa muda mrefu.

Mlinzi huyo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa ameibuka kama mmoja wa mabeki wa Ulaya anaewaniwa zaidi katika misimu ya hivi karibuni na ni sehemu ya timu ya Leipzig ambayo imefungwa mabao 12 tu katika michezo 15 ya Bundesliga msimu huu.
Upamecano, 22, anaonekana kuwa kivutio cha wengi na huenda thamani yake ikazidi kupanda.