Nyota wa Arsenal Mesut Özil ametokea katika kikosi bora cha Arsenal kilichopendekezwa na mashabiki katika mtandao wa Twitter.
Shindano Hilo lijulikanalo kama Twitter Q&A linaendeshwa na Skysport katika mtandao wa twitter wakitaka kujua nini maoni ya mashabiki mbalimbali.
Nyota huyo alitolewa katika kikosi cha Arsenal msimu huu kinachoongozwa na meneja kijana Mikel Arteta, Kwa sasa anahusishwa kuondoka klabuni hapo baada ya kuonekana kutohitajika kikosini hapo.
Baadhi ya timu mbalimbali zimeonesha kupendezwa na kiungo huyo na sasa zikiwa katika makubaliano nae ili kujua hatima yake Kwa washika mitutu hao wa London.