Ule msemo wa wahenga, Ndege wanaofanana huruka kundi moja ndio kilichojiri huko Zanzibar katika mashindano ya kombe la Mapinduzi. Fainali itakayowakutanisha maahasimu wakubwa kutokea Tanzania Huku Simba kule Yanga majira ya saa 2:15 usiku saa za Afrika Mashariki uwanja wa Aman Zanzibar.
Hiyo imetokea baada ya kufuzu timu zote mbili katika hatua ya nusu fainali ambalo Yanga alimtoa Azam Kwa mikwaju mitano ya penati huku Azam wakipata mikwaju minne, baada ya sale ya mojamoja ndani ya dakika tisini. Mchezo wa nusu fainali wa pili uliwakutanisha wababe Simba na Namungo ambapo Simba aliamka kidedea baada ya kumuadhibu Namungo mabao 2-1, na kuwafanya waingie katika hatua ya fainali kukutana na Zanzibar.
Hatua hii Simba na Yanga wanakutana wakiwakosa wachezaji wao muhimu Kwa pande zote mbili walioitwa kulitumikia Taifa katika kikosi cha Taifa stars katika Mchezo wa kirafiki unaowakutanisha Tanzania na DR Congo Leo majira ya saa11:00 jioni uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.
Je?, Nani ataondoka na ndoo awamu hii?.