Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, msanii Joh Maker amesema kwamba ukiachana na EP ya Diamond Platnumz #FOA hakuna EP kali kama ya kwake #MADUBWANA.
“Nimesikiliza Ep Nyingi Saana Zilizotoka Hapa Bongo Ukiachana na #FOA Ep ya Diamond Platnumz Hakuna #Ep Kali Kuliko Yangu #EP Bora Ya Mwaka 2021-2022 #MADUBWANAEP. kuanzia Production imefanyika chini ya Producer Bora wa Mwaka S2kizzy .
“Videos Zimefanyika Chini Ya Kampuni Kubwa Ya Director Bora Wa Mwaka @hanscana_ #hanscanabrand Cc; @director_joma Bila Kusahau Hakuna Management, Hakuna Kazi Nyingine Nafanya Zaidi Ya Mziki ,na Kuna Wakati Hatuonekani Kwenye Events,Clubs n.k ilimradi Tuweze Kumake Hela Za Kushoot Videos na Kuachia Projects Bora Zaidi Ambazo Tunaimani Zitakuja Kubadili Maisha Yetu Nasisi Na Familia Zetu Tuagane na Umasikini.
“Inaeleweka Nowdays Kwamba Habari Binafsi Ya Msanii Ni Biashara ila Tukumbushane Pia Mziki Wa Msanii Nao Ni Biashara So Ombi Langu Kwa Yeyote Anayehusika na Ujumbe Huu Tusichukuliane Poa Kwenye Hiki Tunachokifanya Maana Tunatumia Nguvu ,Akili na Tunajua Muda Unaenda na Umri Unaenda. Swali la Kujiuliza; Ajira Kwa Vijana Hakuna Na Kwenye Kujiajiri Kupitia Vipaji Vyetu Hatupati Tunachostahili Je, Kesho Mtatufunga Jela Mkitukuta Chocho Tunawakaba Hiyo Mishahara Yenu?