Msanii wa Bongofleva Harmonize, ametangaza ujio wa Afro East Carnival Season 2 ambayo itafanyika pale Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, May 29, 2022.
Harmonize amesema atajitaidi kuwaleta wasanii wengi alioshirikiana nao wa nje ya nchi ambao hawakuepo mara ya kwanza kwani changamoto kubwa waliyokutana nayo mwanzoni ni kushindwa kufanya mpango wa visa mapema.
Viingilio vya Tamash hilo vinaanzia Elfu 5 hadi Elfu 10 na kutakuwa pia na VIP. “Sababu ya kufanya Season 2 DSM ni kwasababu naamini kuna watu wengi hakuwagusa kwenye Tamasha la kwanza hivyo nawaletea hili la pili ili mashabiki wangu wote wapate burudani na baada ya hapo itaenda mkoani”