Baada ya kuondoka katiak lebo ya Konde Gang, rapa Country Boy amefungua Record label na Music Company iliyopewa jina la iam music .
Country Boy amethibitisha hilo kupitia katiak ukurasa wake wa mtandao wa kijaamii wa Instagram kwa kuandika
“Kutokana na jitihada anazozionesha Rais wetu mpendwa, mama etu kipenzi MH. SAMIA SULUHU HASSAN kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele mimi kama kijana sijataka kubaki nyuma. Nimefungua kampuni iitwayo @iam_music_co ambayo itahusika katika kusaidia vijana Mtaani ambao wengi wanataman kutimiza ndoto zao lakin wanashindwa kutimiza kutokana Na changamoto wanazokutana nazo hvyo basi Nakuja mbele yenu Watanzania na serikali kwa ujumla kuipokea KAMPUNI hii..”Hatuna pesa nyingi lakin Tunaamin katika kidogo tulichonacho Kitatuvusha kutoka sehem Moja kwenda Nyingne🙏🏿