Staa wa Muziki Nchini Harmonize Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Ametoa Ufafanuzi kuhusu Tamasha la Afroeastcarnival Season two.
–
Harmonize amesema kuwa Tamasha hilo linalotarajiwa Kufanyika Mei 29,2022 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam kuwa hakutokuwa na Wasanii wengine Tofauti na yeye kama ilivyokuwa Tamasha la kwanza lililofanyika Tabata Shule na kuwa na List ya Wasanii wengi waliotangazwa kutumbuiza kwenye Tamasha hilo.
–
Lakini pia Staa huyo Amesema katika Tamasha hilo atatumia Masaa 4 jukwaani na atatumbuiza nyimbo 60 na kutakuwa na Suprise nyingi ambazo hazitotangazwa.