Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha Clouds Fm mwanamitindo Hamisa Mobetto amesema
“Nilishawahi kutolewa posa mara nyingi sana na wengine siwafahamu na wengine nawafahamu lakini unakuta mambo hayajakaa sawa maana suala la ndoa ni la kujipanga. Posa ndogo ambayo ilishawahi kuja nyumbani ilikuwa million kumi.
Mimi nina watoto na nimekuwa kwenye mazingira ya kushuhudia baadhi ya ndugu zangu wananyanyasika sababu hawana na chao hivyo kabla sijaingia kwenye ndoa nataka nijikamilishe ili hata nikiingia niwe full na hata miaka ya mbele ikishindikana basi niwe na vyangu” Hamisa Mobetto