Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo, 37, anatazamia kuondoka Manchester United, huku Roma ya Jose Mourinho na Sporting Lisbon zikivutiwa naye .
–
Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel angependa kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29 – ambaye analengwa na Inter Milan – na mshambuliaji wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 33 wa Poland Robert Lewandowski, lakini kuna vikwazo muhimu katika kukamilisha mikataba yote miwili.
–
Lewandowski anayelengwa na Barcelona anasema bado anataka kuondoka Bayern lakini hataki kuharibu uhusiano wake na klabu hiyo ya Ujerumani kwa kulazimisha uhamisho
–
Tottenham wapo mstari wa mbele kumsajili mlinzi wa Middlesbrough Muingereza Djed Spence, 21, huku Nottingham Forest ikikubali kuwa huenda asijiunge nao, baada ya kukaa kwa mkopo City Ground msimu uliopita.
–
Sevilla wako tayari kutoa £6.9m kwa mshambuliaji wa Rangers na Colombia Alfredo Morelos, 25.
–
est Ham wako tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Croatia Nikola Vlasic, 24, huku Hadjuk Split na Torino wakimtaka.
–
Manchester United wana imani Barcelona itapunguza bei yao ya pauni milioni 73 ili kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kwa sababu ya matatizo yao ya kifedha.