Mwanadada mmoja anayeishi maeneo ya Mikocheni B, jijini Dar es Salaam atapeliwa simu yake ya mkononi aina ya Iphone yenye thamani ya Tsh.900,000/= na kijana mmoja aliyejitokeza mahali pasipojulikana kisa uhitaji wa nafasi ya kufanya kazi kwenye duka la nguo tukio liianza kama ifuatavyo; kijana huyo alimuuliza yule dada kama anahitaji kazi ya kuuza duka la nguo maeneo ya Sinza, mwandada alikubali kwa kusema anahitaji kazi hiyo, hivyo kijana yule akapata nafasi ya kumuazima simu ili aweze wasiliana na mtu aliesemekana ndie bosi anayemiliki duka hilo, akazuga kwa muda mfupi kama anawasiliana na mtu kisha akaita bodaboda na kumwambia dada huyo waongozane pamoja hadi huko duka lilipo, walipofika Sinza kaatika eneo husika yule dada alishajijenga imani ya kuwa huyo kijana ni mwaminifu tu bila ya kujua kuna kamchezo kana endelea akamwachia bado atumie simu yake ya Iphone ili kuwasiliana na mtu anayehusika na utoaji wa ajira mwishowe yule kijana akateremka kutoka kwenye pikipiki huku akizuga anawasiliana bado na mtu kisha akawambia kwapamoja wamsubiri pale nje wakiwa katika pikipiki kwani anarejea na bosi wake muda sio mrefu, kijana alipoondoka akazamia hukohuku muda ulipozidi kusogea ndipo yule deeva wa bodaboda ikabidi amuulize yule mdada mbona huyo mwezio harejei na kwani unamjua?, mwanadada akasema hata simjui kuseama ukweli, boda akasema sasa mbona umemwachia simu mtu usiemjua na hatokei utakuwa umeshatapeliwa hapo na mimi pesa yangu anatalipa nani, hapo yule dada ikabidi aombe msamaha tu kwa boda boda kisha kutafuta raia wema waweze msaidia nauli aweze kurudi Mikocheni B alipokuwa.
TANZANIA, UAE ZASAINI KUHIFADHI MAZINGIRA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe, Dkt. Selemani Jafo amesema biashara ya kaboni itasaidia...
Read more