Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA inatoa nafasi ya ukaribisho kwa wananchi mbalimbali kwenda kutembelea banda lao katika maonesho ya Sabasaba yanayofanyika katika viunga vya Sabasaba wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam ili kuweza pata elimu ya mlipakodi kama ilivyoelezwa na mkurugenzi wa huduma na elimu ya mlipa kodi TRA Bw.Richard Kayombo.