Mtendaji mkuu wa Manchester United Richard Arnold na mkurugenzi wa ufundi John Murtough wako Barcelona kujaribu kukamilisha usajili wa kiungo mholanzi Frenkie de Jong, 25. (Manchester Evening News)
Kiungo wa Leicester City na Ubelgiji Youri Tielemans, 25, na kiungo wa Wolves mreno Ruben Neves, 25, wanasakwa na Manchester United iwapo watashindwa kumnasa De Jong. (Talksport)
Barcelona imekubali kutoa ada wanayotaka Leeds United ya £65m kwa ajili ya kiungo Mbrazil Raphinha, 25, na kipaumbele cha sasa cha klabu hiyo ya Hispania ni kumuuza De Jong kwenda Manchester United. (Mirror)
Chelsea inaonekana iko nyuma ya Barcelona kwa sasa kwenye mbio za kumsaka Raphinha ambapo badala yake “the Blues” huenda wakamgeukia winga wa Bayern Munich na Ujerumani Serge Gnabry. (Mail)
Mkataba wa mshambuliaji mfaransa Ousmane Dembele pale Barcelona umeisha, lakini nyota huyo mwenye miaka 25 anatarajia kusaini mkataba mpya kusalia Nou Camp utakaokwenda mpaka 2024. (Marca)
Wolves imekataa ofa ya £25m kwa ajili ya kiungo muingereza Morgan Gibbs-White, 22, kutoka Everton. (Mail)