Rais Samia Suluhu Hassan Jumatano, Julai 20 amemteua Camilius Wambura kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Tanzania. Kabla ya uteuzi wake Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI). IGP mpya anachukua nafasi ya Simon Sirro ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Sirro aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam aliteuliwa kuwa mkuu wa polisi Mei 29, 2017 akichukua nafasi ya Ernest Mangu. Katika uteuzi wa hivi punde, Kamanda Mkuu wa Majeshi pia alimteua Ramadhan Hamisi Kingai kuwa Mkurugenzi mpya wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI). Katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais iliyotolewa alfajiri ya Jumatano, walioteuliwa hivi karibuni wanatarajiwa kuapishwa leo katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre ameonya Wabunge wa Bunge la Uganda kwamba vikwazo vitakavyowazuia kufanya biashara na Marekani...
Read more