Zikiwa zimesalia siku 5 kuelekea siku rasmi ya Kufanya NBC Dodoma Marathon, Benki ya Taifa ya Biashara bado ipo katika muendelezo wa mchakato wa usaji wa washiriki wa mbio hizo zitakazofanyika makao makuu ya Nchi jijini Dodoma Julai 31, 2022 hivi karibuni wametuma jumbe zao kupitia kurasa za mitandao ya kijamii kuwa wapo maeneo ya Mlimani City Mall wakiendeleza zoezi hilo na watakuwepo hadi saa 3 usiku muda wa saa za Afrika mashariki.
“Bado tupo Mlimani City Mall mpaka saa 3:00 Usiku.
Karibu ili uweze kujisajili na kuchukua kifurushi chako cha #NBCDodomaMarathon2022 papo hapo.
Unaanzaje kukosa kushiriki Marathon ya Kimataifa”.