
Benki ya NBC yazindua kadi inayowezesha malipo mtandaoni kwa njia ya Dola. Kupitia kadi hii wateja wanapata fursa ya kufanya malipo ya bidhaa na huduma kwa dola pasipo makato ya ziada.
Ni mapinduzi ya tehama yanayowezesha malipo ya visa kadi inayohakikishia wateja usalama na urahisi pindi wafanyapo malipo ya mtandao.
Mbali na kumwezesha mtumiaji wa kadi hiyo kufanya malipo ya mtandaoni bila malipo ya ziada, kadi hii pia ina uwezo wa kutumika kwenye makampuni ya Visa zaidi ya 2000(ATM) kwa Tanzania, zaidi ya kampuni milioni 2.7 za Visa Duniani kote na pia zaidi wafanyabiashara 24,000 wanaopokea malipo ya Visa kwa Tanzania.