
Tumezindua tawi jipya lililopo Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar, kukusogezea huduma mbali mbali za kibenki karibu yako, Tawi hili limezinduliwa leo tarehe 25/07/2022, na Raisi wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.
Sambamba na uzinduzi wa tawi hili pia tumekabidhi pikipiki na boti za uvuvi na kilimo Ili kuwashirikisha wananchi wengi katika kuujenga uchumi wa buluu visiwani humo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi Rais Dkt. Hussein Mwinyi alisema
“Tawi hili linatoa huduma za benki kwa masharti ya Kiislam na yale ya kawaida. Serikali kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuwawezesha wananchi kiuchumi ndio maana inasogeza huduma zikiwamo za kifedha jirani yenu. Kila mmoja aangalie fursa zilizopo kukuza uchumi wake,”
Sherehe za uzinduzi zimehudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji, Bw. Abdulmajid Nsekela,Viongozi mbalimbali, wafanyakazi wa benki ya CRDB pamoja na wananchi.
Unachostahili ni huduma popote ulipo

