
Idadi ya vifo vya wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la Shule ya Msingi King David iliyotokea leo mkoani Mtwara imeongezeka na kufika tisa na kufanya idadi ya jumla waliofariki katika ajali hiyo kufikia 11.
Miili ya wanafunzi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula ya mkoani Mtwara na majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma hospitalini hapo.
