Ikiwa zimesalia siku 4 kuelekea Riadha ifaamikayo kama NBC Dodoma Marathon iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara NBC, benki hio imeamuakuongeza kituo kwaajili ya kurahisisha wadau kujisajiri na kupata huduma zihusianazo na mbio hizo zitakazofanyika jijini Dodoma siku ya Jumapili Julai 31,2022 ikijumuisha umbali wa mbio tofauti ambazo ni kilometa 5K,10K,21K, na 42K ambapo washiriki watakaoshinda watajinyakulia fedha taslimu zilizotolewa kama zawadi na benki hio.











