Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong angeondoka tu Barcelona kwenda Chelsea lakini klabu hiyo ya London haiko tayari kulipa kiasi cha Manchester United kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sport – in Spanish)
Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo anasema hajui ni nani “aliyebuni” hadithi inayomhusisha mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo na timu ya Uhispania na kwamba “haiwezekani” mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 37 kujiunga nao. (El Partidazo de COPE, via Eurosport)
Newcastle United wanavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 26. (Christian Falk,Bild)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Juventus watamtazama mshambuliaji wa Werner na Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, kama hawataweza kukamilisha kumnasa mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 29, kutoka Atletico Madrid. (Sky Sports)
Matumaini ya Tottenham kumnunua kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 23, yanaweza kuathiriwa baada ya mchezaji mwenzake wa Juventus, Paul Pogba, wa Ufaransa, 29, kupata jeraha la goti. (Mail)
Chelsea wameelekeza mawazo yao katika kujaribu kumsajili beki Mholanzi Denzel Dumfries, 26, kutoka Inter Milan baada ya kutatizika kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Jules Kounde, 23, kutoka Sevilla. (Evening Standard)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mkufunzi wa Barcelona Xavi anasema “haiwezekani” kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kwa sasa kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 yuko chini ya mkataba na Paris St-Germain lakini akaongeza kuwa “tutaona katika siku zijazo”. (Goal)
Mlinda mlango wa Leicester City Kasper Schmeichel amekubali kujiunga na klabu ya Nice ya Ufaransa lakini uhamisho huo haujaidhinishwa kwani Foxes bado hawajapata mbadala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 35. (L’Equipe – in french)
Mwenyekiti wa Leicester City Aiyawatt Srivaddhanaprabha anasema klabu hiyo haikuwa na ofa yoyote kwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye mkataba wake na Foxes unamalizika msimu ujao wa joto. (Metro)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Crystal Palace, Leicester City na Newcastle United wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Strasbourg Mfaransa Ludovic Ajorque, 28. (Football Insider)
Everton wanavutiwa na beki wa kushoto wa Sporting Lisbon Ruben Vinagre, 23, ambaye aliwahi kuichezea Wolves. (Liverpool Echo)
Southampton wamefanya uhamisho wa kuchelewa kujaribu kumsajili winga wa Manchester City Muingereza Sam Edozie, 19, ambaye alitarajiwa kujiunga na Bayer Leverkusen. (Mail)
Burnley wamekuwa na ofa ya pauni milioni 1.5 kwa winga wa Ubelgiji Manuel Benson, 25, iliyokataliwa na FC Antwerp. (Mail)