Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi akimkabidhi funguo mshindi wa Bajaj wa promosheni ya Vodacom “M-Pesa Imeitika” kutoka Morombo jijini Arusha, Mwanaisha Nyonyo Mohamed wakati wa hafla ya wiki ya kwanza iliyofanyika kwenye viwanja vya Soko la Kilombero jijini humo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, Abednego Mhagama. Vodacom inatoa zawadi ya bajaj moja na bodaboda nne (zote mpya) kila wiki kwa wiki nane ili kuhamasisha matumizi ya pesa kidijitali. Zawadi kuu itakuwa ni nyumba mpya iliyosheheni samani zote. |